Baada ya kushinda michezo 18
mfululizo ya Ligi Kuu ya Uingereza, hatimaye Crystal Palace
imefanikiwa kusimamisha rekodi ya ushindi wa Manchester City hii leo.
Crystal Palace licha ya kutoa sare
tasa na vinara wa ligi Manchester City, pia ingeweza kuibuka na
ushindi wa goli moja lakini kipa Enderson aliwanyima ushindi.
Palace walidhani kuwa wataibuka na
ushindi baada ya kupata penati dakika za mwisho baada ya kuangushwa
Wilfred Zaha lakini penati ya Luka Milivojevic ilipanguliwa.
Licha ya kutibuliwa rekodi ya
ushindi mfululizo Manchester City pia imejikuta ikikumbwa na hofu ya
majeruhi baada ya Kevin De Bruyne na Gabriel Jesus kuumia.
Raheem Sterling akimuangusha katika eneo hatari Wilfred Zaha na muamuzi kuamua mkwaju wa penati
Luka Milivojevic akishuhudia mpira wa penati aliyoipiga ukizuiliwa kwa miguu na kipa Enderson wa Manchester City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni