Kiungo Mfaransa Corentin Tolisso
amefunga mara mbili na kuipatia Bayern Munich ushindi wa magoli 3-1
dhidi ya Paris St-Germain katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya
uliopigwa jana usiku.
Bayern ilikuwa ya kwanza kufunga
goli kupitia kwa Robert Lewandowski katika dakika ya nane, Talisso
akaongeza la pili kabla ya Kylian Mbappe akachomoa moja kisha Talisso
akafunga la tatu.
Robert Lewandowski akiifungia Bayern Munich goli la kwanza
Timu ya Chelsea imelazimisha sare ya
1-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya
uliochezwa jana usiku.
Chelsea iliutawala mchezo huo hadi
pale ilipofungwa goli la kwanza na Saul Niguez katika dakika 56
kufuatia shambulizi la Fernando Torres.
Saul Niguez akiifungia Atletico Madrid goli kwa mpira wa kichwa katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni