Jose Mourinho amesema timu
hazitofurahia zikipangwa kukutana na Manchester United katika hatua
ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga jana CSKA Moscow
2-1.
Katika mchezo huo Manchester United
ilitokea nyuma na kujihakikishia kutinga hatua ya 16 bora ikiwa ni
mara ya kwanza kufikia hatua hiyo tangu David Moyes alipokuwa kocha.
CSKA Moscow ya Urusi ilikuwa ya
kwanza kufunga goli kupitia kwa Vitinho katika kipindi cha kwanza
lakini Romelu Lukaku akasawazisha kisha Marcus Rashford akaongeza la
pili.
Mshambuliaji Marcus Rashford akiifungia Manchester United goli la pili
Romelu Lukaku akijaribu kufunga goli kwa kujirusha mithili ya sarakasi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni