.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 6 Desemba 2017

KILIMANJARO WAPONGEZWA KWA KUZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI

MKOA wa Klimanjaro, umepongezwa kwa kuitikia agizo la Rais John Magufuli la kutaka kila mkoa ubainishe fursa za uwekezaji zilizopo na kuandaa mwongozo wa uwekezaji.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Kilimanjaro uliondaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Akimwakilisha Waziri wa Nchi wa Ofisi hiyo Selemani Jafo, Naibu Waziri huyo alisema kwamba agizo la Rais ambalo limelenga kuweka mikakati mahsusi ya kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda.

Akitoa salamu za pongezi kwa Mkuu wa mkoa, Mh. Anna Mghwira Naibu Waziri Kakunda alisema wakati mkoa wa Kilimanjaro unatekeleza maagizo, serikali kuu nayo inaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ili kuvutia wawekezaji mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mh. Joseph Kakunda akitoa hotuba wakati wa kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro kwa niaba ya Waziri wa Nchi wa Ofisi hiyo, Mh. Selemani Jafo (hayupo pichani) kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la NSSF mjini Moshi, mkoani humo.

Akizungumzia Mwongozo huo Naibu Waziri alisema kwamba kazi ya kubaini fursa za uwekezaji katika miradi mbalimbali yenye faida siyo tu kwa wawekezaji pekee bali pia kwa taifa letu kupitia kodi na upatikanaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa kila eneo la nchi.

Alisema kazi iliyofanywa na mkoa huo ina maana kubwa kwa kuwa sasa inakuwa rahisi kwa wawekezaji wawe wa ndani au nje kujua namna ya kuwekeza katika mkoa wa Kilimnjaro kwa kuzingatia mahitaji yao na namna rasilimali watu na miundombinu ilivyo.

Alisema agizo la Rais la utengenezaji wa mwongozo unakwenda sanjari na ubainishaji na uandazi wa maeneo ya uwekezaji ili yanapotakiwa yapatikane hima.
Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mh. Joseph Kakunda (katikati) kutoa hotuba ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour.

Aliutaka mkoa huo kuutangaza mwongozo wao kwani biashara ni matangazo katika maeneo mbalimbali ya kimataifa na ya wawekezaji katika masoko ya hisa kwa njia ya kielektroniki ili wavune utayari wao wa kukaribisha uwekezaji.

Kakunda alisema kwamba mkoa huo kwa asili unaweza kabisa kuvutia wawekezaji. Kinachostahili kufanywa kwa sasa ni kuhakikisha kauli mbiu ya Kilimanjaro ya Viwanda, inawezekana chukua hatua inatekelezwa kwa vitendo.

Akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira alisema kwamba Mwongozo huo utafanyiwa kazi na matunda yake yataonekana wakati taifa linaelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Alisema mkoa huo una rasilimali za kutosha kuwezesha wawekezaji mbalimbali kutekeleza adhma ya kuwa na viwanda vidogo na vya kati vinavyotumia rasilimali kutoka mkoani.

Aliwashukuru wataalam wa ESRF waliwezesha kupatikana kwa muongozo huo na wafadhili ambao ni UNDP.

Naye Dk Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ambayo ndiyo ilipewa jukumu na Mkoa wa Kilimanjaro kufanya utafiti na uchambuzi wa kina ili kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa, aliupongeza mkoa wa Kilimanjaro kwa kuona umuhimu wa kuwa na mwongozo wa uwekezaji.

Aidha katika hotuba yake hiyo alisema kuwa taasisi yake ilitengeneza sehemu tatu za taarifa ambazo zote zililenga kutoa uwanda mpana kwa wawekezaji kuwa na taarifa muhimu za uwekezaji katika mkoa wa Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Mbaga Kida akitoa taarifa kuhusu uandaaji wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na taasisi yake kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) katika hafla iliyofanyika mjini Moshi kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF.

Alisema katika hotuba yake kwamba ESRF ilifanikiwa kuandaa ripoti tatu ambazo ni Ripoti ya Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials Report), Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities Report) pamoja na Mwongozo wa Uwekezaji ambao Mkoa umezindua rasmi leo.

Pia alisema kwamba Ripoti hizo zilithibitishwa na Mkoa Oktoba 12, 2017 katika warsha maalum iliyoandaliwa na Mkoa wa Kilimanjaro.

Mapema mwaka huu Mwongozo kama huo ulizinduliwa Mkoani Simiyu ambao umeleta matokeo makubwa ndani ya muda mfupi. Wiki mbili zilizopita mkoa wa Mwanza nao ulizindua mwongozo wa uwekezaji. Mkoa wa Mara katika siku za usoni unatarajiwa kuzindua mwongozo wa uwekezaji. Miongozo yote hiyo imeandaliwa na ESRF.

Alisema miongozo hiyo ya Uwekezaji inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016 – 2021) unaosisitiza ujenzi wa Tanzania ya Viwanda ili kuifikisha nchi katika uchumi wa kati ifikapo 2025.
Sehemu ya wadau wa sekta binafsi, serikali, wawekezaji na taasisi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na UNDP kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.

Katika hotuba yake pia Dk Kida aliiushukuru Uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa Mkoa, Anna E. Mghwira, Katibu Tawala wa Mkoa, Mhandisi Aisha S. Amour na viongozi wengine wa mkoa na wilaya zote kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu wakati wanapita kutafuta maoni.

Aidha alitoa shukurani kwa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ufadhili wa fedha.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa nne kulia), Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (wa tatu kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira (wa nne kushoto), Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (wa tatu kulia) Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF Bi. Margareth Nzuki (wa pili kulia), Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Hoseana Lunogelo (kulia), Watafiti vijana kutoka ESRF Bw. Mussa Martine (kushoto) pamoja na Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Pia alishukuru timu ya ESRF ikiongozwa na Bi. Margareth Nzuki, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu kwa kuratibu, watafiti washiriki Prof. Haidari Amani; Dkt. Hoseana Lunogelo na Prof. Samuel Wangwe kwa kupitia mwongozo huu.

Aidha aliwashukuru watafiti vijana Bw. Mussa Martine, Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani pamoja na Bw. John Shilinde. Aidha, alisema anatambua mchango mkubwa aliotoa marehemu Abdallah Hassan katika uandaaji wa Mwongozo huu.

Pia alisema ESRF ipo kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi wake na hivyo wasisite kuwatumia pale wanapohitaji msaada wa kitaalam.
Mshiriki Mtafiti wa ESRF, Dkt Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji mkoani Kilimanjaro zilizoonekana wakati wa kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwongozo huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Hoseana Lunogelo (katikati) pamoja na Watafiti vijana kutoka ESRF Bw. Mussa Martine (kulia) pamoja na Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na UNDP.
Picha juu na chini baadhi ya wadau na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi, mkoani humo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua rasmi Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia) wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akionyesha nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuzindua rasmi huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia) wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akikabidhi nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa Mkuu wa mkoa huo, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto) mara baada ya kuzindua rasmi huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) amoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia) wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Mbaga Kida akipeana mkono na Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi wakati wa kukabidhi nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Kilimanjaro na wadau wa maendeleo Ubalozi wa Uholanzi na taasisi zingine huku wakiwa wameshika nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya mkoani Kilimanjaro.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za serikali.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika picha ya pamoja na baadhi ya wawekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika picha pamoja na Sekretarieti ya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkuu, Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika picha ya pamoja na Bendi ya Chuo cha Polisi Moshi (CCP) waliokuwepo ukumbini hapo kusherehesha uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro.
Kaimu Mkurgenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Bw. Primus Kimaryo akizungumza na kuelezea kuhusu kazi za Bodi ya Kahawa nchini mara baada ya kuzinduliwa rasmi Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
Kaimu Meneja wa Kanda wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Bw Brendan Maro akitoa salamu za TIC katika kuelekea Kilimanjaro ya Viwanda wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda pamoja na Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira wakiimba wimbo wa 'Tanzania Yetu' wakishirikiana na bendi ya Chuo cha Polisi Moshi (CCP) iliyokuwa ikisherehesha uzinduzi huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni