Timu ya Chelsea imeendeleza wimbi la
ushindi katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya hii leo kuibuka na
ushindi wa kishindo wa magoli 5-0 dhidi ya Stoke City na kumaliza
mwaka 2017 kwa ushindi.
Katika mchezo huo wenyeji Chelsea
walifunga goli la kwanza kupitia kwa Antonio Rudige kufuatia krosi ya
Mbrazil Willian kisha baadaye Danny Drinkiwater akaongeza goli la
pili kisha Pedro akafunga la tatu.
Willian aliongeza goli la nne kwa
mkwaju wa penati baada ya kuchezewa rafu na Geoff Cameron na katika
dakika ya 88 Zappacosta akakamilisha karamu ya magoli kwa kufunga
goli lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza.
Antonio Rudige akifunga goli la kwanza la Chelsea katika mchezo huo
Danny Drinkwater akifunga kwa shuti la kuubetua mpira kwenye kona ya goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni