Raia wa Misri Mohamed Salah amefunga
magoli mawili na kuisaidia Liverpool kuongeza rekodi yao ya
kutofungwa katika michezo 15 kwenye michuano yote baada ya kuibuka na
ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Leicester City.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye
dimba la Anfield Jamie Vardy aliwapatia wageni goli la kuongoza
akiitumbukiza kiulani pasi ya Riyad Mahrez goli lililoduma hadi
kipindi cha pili pale Salah alipoisawazishia Liverpool.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri
baadaye tena alimzungusha Harry Maguire na kuachia shuti lililojaa
wavuni na kuandika goli la pili na kufikisha magoli 17 katika michezo
ya Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu huu.
Mshambuliaji nyota wa Leicester City akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Mshambuliaji nyota wa Liverpool Mohamed Salah akifunga goli la kusawazisha kabla ya baadaye kuongeza la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni