Alvaro Morata amefunga goli la
dakika za majeruhi na kuifanya Chelsea kutinga hatua ya nusu fainali
ya Kombe la Carabao kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Bournemouth.
Willian alifunga goli la kwanza
kufuatia shambulizi nzuri ambalo liliishia kwa Cesc Fabregas kutoa
pasi ya mwisho kwa Willian.
Bournemouth ilifikiria kuwa mchezo
huo ungeingia katika dakika za ziada baada ya Dan Gosling kufunga
goli la kusawazisha lakini Morata aliyetokea benchi akaongeza la
pili.
Dan Gosling akifunga goli la kusawazisha hata hivyo Chelsea waliongeza goli la ushindi baadaye.
Mshambuliaji Alvaro Morata aliyetokea benchi akifunga goli la ushindi la Chelsea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni