Mchezaji Korey Smith amefunga goli
la dakika za majeruhi wakati timu ndogo ya Bristol City ikiwatoa
mabigwa watetezi wa kombe la Carabao Manchester United kwa magoli
2-1.
Smith alifunga goli katika dakika ya
mwisho ya mchezo huo na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ambapo
sasa watavaana na Manchester City.
Bristol City walikuwa wa kwanza
kufunga goli kupitia kwa Joe Bryan lakini goli hilo lilidumu kwa
dakika nane kabla ya Zlatan Ibrahimovic kusawazisha.
Zlatan Ibrahimovic akiachia shuti na kufunga goli pekee la Manchester United katika mchezo huo
Korey Smith akifunga goli la ushindi lililowaondoa mabingwa watetezi Manchester United
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni