Mshambuliaji wa Real Madrid,
Cristiano Ronaldo, amekuwa mchezaji wa kwanza kuifungia magoli timu
yake katika michezo yote ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika
msimu wakati wakiifunga Borussia Dortmund magoli 3-2.
Cristiano Ronaldo aliachia shuti
zuri na kufunga goli hilo lililomfanya kuweka rekodi nyingine na
kufikisha magoli tisa katika michuano hiyo msimu huu wakati mabingwa
hao watetezi wakitinga hatua ya 16 bora.
Ronaldo ameshafunga jumla ya magoli
114 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akimpita Lionel Messi
wa Barcelona kwa tofauti ya magoli 17. Real Madrid inanafasi kwa
asilimia 50 kukutana na timu ya Uingereza katika hatua ya 16 bora.
Kipa wa Borussia Dortmund akibaki anauangalia mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo ukijaa wavuni
Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli kati ya magoli yake mawili aliyoifungia Borussia Dortmund
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni