.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 7 Desemba 2017

TOTTENHAM YAEDELEA KUFANYA VIZURI LIGI YA MABINGWA ULAYA


Tottenham imemaliza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya bila ya kufungwa baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Apoeli Nicosia.

Fernando Llorente aliifungia Tottenham goli lake la kwanza katika michezo 17, huku magoli mengine ya timu hiyo yakifungwa na Son Heung-min pamoja na Georges-Kevin N'Koudou.

                                         Fernando Llorent akiifungia Tottenham goli la kwanza
Timu ya Manchester City imepoteza mechi yake ya kwanza kati ya michezo 29, huko Ukraine baada ya kufungwa na Shakhtar Donetsk magoli 2-1 hata hivyo imetinga hatua ya 16 bora katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo Manchester City ambayo inaongoza kundi hilo ilijikuta ikifungwa goli la kwanza na Bernard kwa shuti la kuzungusha, Ismaily akaongeza la pili huku Sergio Aguero akaifungia goli pekee kwa penati.
                Kocha wa Manchester City Pep Guardiola akiinamisha kichwa chini baada ya kichapo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni