Philippe Coutinho amefunga magoli
matatu yaani hat-trick wakati Liverpool ikiwa klabu ya tano ya
Uingereza kutinga hatua ya 16 bora katika Ligi ya Mabinwa Ulaya.
Katika mchezo huo Liverpool
iliichakaza bila ya huruma timu ya Spartak Moscow kwa magoli saba
bila ya majibu katika dimba la Anfield.
Magoli mengine ya Liverpool
yalifungwa na Roberto Firmino, Msenegali Sadio Mane akitupia mawili
naye Mohamed Salah akafunga goli moja.
Roberto Firmino akifunga goli katika mchezo huo wa jana usiku
Msenegal Sadio Mane akifunga goli licha ya kuanguka chini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni