Nyota mkongwe wa soka duniani Diego
Maradona ametambulisha sanamu yake akiwa ameshikilia kombe la dunia
nchini India.
Mchezaji huyo anayeheshimika katika
mji wa Kolkata ametambulisha sanamu hiyo baada ya kuhairisha mara
kadhaa shughuli hiyo.
Katika hafla hiyo Maradona
amesisitiza kwa masahabiki hao wa India wanaomhusudu mno kuwa yeye si
Mungu bali ni mchezaji soka tu.
Mbali na uzinduzi wa sanamu Maradona
alitoa hundi kwa wagonjwa 11 wa saratani pamoja na kukabidhi gari la
wagonjwa.
Sanamu ya Diego Maradona iliyozinduliwa mjini Kolkata nchini India
Nyota mkongwe wa soka Diego Maradona akiweka saini yake kwenye mpira
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni