.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 9 Desemba 2017

“HITILAFU YA UMEME YAUNGUZA BAADHI YA VIFAA OFISI YA ELIMU SEKONDARI JIJI LA TANGA”

Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto naUokoaji mkoa wa Tanga, Inspekta Kumenya Bakari akizungmza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji wakitoa vitu nje kwenye ofisi ya Elimu Sekondari ya Jiji hilo baada ya kuungua kutokana na hitilafu ya umeme.

HITILAFU ya Umeme iliyotokana na mgandamo wa hewa imesababisha ofisi ya Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Tanga kuungua moto ikiwemo baadhi ya vitu vilivyo kuwemo ndani kabla kuzimwa ili usiweze kusambaa kwenye maeneo mengine ndani ya Halmashauri ambao ungeweza kuleta athari kubwa.

Jitihada za kuufanya moto huo usiweze kusambaa kwenye maeneo mengine ulifanywa na watumishi wa halmashauri hiyo ambao walitumia vifaa
vya kuzimia moto huo baada ya kupatiwa elimu ya kupambana na majanga ya moto.

Akizungumza jana,Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Tanga, Inspekta Kumenya Bakari alithibitisha kuungua kwa ofisi hiyo
ambapo alisema tukio hilo lilitokea Desemba 8 asubuhi saa tano asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa kijana wa boda boda na ndipo walipoamua
kutoka na magari yao.

Alisema pamoja na kupewa taariufa hizo wakiwa wanajiandaa kufika eneo la
tukio wakasikia alamu iliyopo ofisini iliwaonyesha kuna moto unawaka
eneo la ofisi ya halmashauri na ndipo vijana wakatoka kwa haraka sana
pamoja na askari waende kuona na kuchukua hatua ya kuuzima.

Aidha alisema ushupavu wa watumishi hao kuwahi na kuuzima moto huo kwa
kuanzia na uzimaji wa swichi kubwa ya umeme inatokana na elimu ambayo
walikwisha kuwapatia namna ya kukabiliana na majanga ya namna hiyo pindi
yanapotokea kwenye maeneo yao na hivyo kuweza kuuzima mapema.

Naye kwa upande wake,Msaidizi wa Afisa Habari wa Kikosi hicho mkoani
Tanga,Sajenti Mussa Msengi alisema baadhi ya vitu ambavyo vimeungua
niSimu moja,pazia, Fax Mashine, Printer, Meza , Rimu na Nyaraka
mbalimbali zilizokuwemo ndani ya ofisi hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Alhaj Mustapha Selebosi alisema baada ya kutokea tukio hilo watakachokifanya hivi sasa ni kurekebisha kutokana na kuwepo kwa vitu vingi ambavyo vimejaa hivyo kunaweza kupelekea matukio ya namna hiyo.

Alisema iwapo wasingekuwa na mitambo yao ya kuzimia moto inaweza
kupelekea hasara kubwa kwa kuungua jengo lote.

“Kwanza nishukuru kuwepo kwa mitambo yetu wenyewe ya kuzimia moto hasa
yanapojitokeza majanga ya moto ni moja kati ya vitu muhimu vilivyosaidia
kukabiliana na janga hili “Alisema.

MBUNGE WA TANGA ASHIRIKI KUUZIMA MOTO.

Awali akizungumza na gazeti hili,Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku  alikuwa ni miongoni mwa watu walioshiriki kwenye
zoezi la kuuzima moto huo ili usiweze kuleta madhara katika maeneo
megine.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo,Mbunge Mussa alisema
ipo haja halmashauri kuongezwe vifaa vya kuzimia moto lakini pia kuwepo
na alama ambazo zitakuwa zikitoa ishara wakati yanapojitokeza mambo ya
namna hiyo.

"Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana wakati wa tukio hili linatokea kwa
sababu na mimi nilikuwepo na nimeshuhudia lakini niseme upo umuhimu
mkubwa kuwepo kwa vifaa vya kutosha vya kuzimia moto katika maeneo
mbalimbali ya majengo ya serikali kuweza kunusuru na hasara zinazoweza
kutokea kama ilivyokuwa leo (jana) tulivyoweza kupambana na moto na
kuuzima "Alisema.
                                   
                                    Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni