West Ham imeshinda mchezo wake wa
kwanza ikinolewa na kocha David Moyes wakati Marko Arnautovic
akifunga goli lake la kwanza kwa klabu hiyo na kuibuka na ushindi wa
goli 1-0 dhidi ya Chelsea katika dimba la London.
Wagonga nyundo hao wa Jiji la London
walifunga goli hilo pekee katika mchezo huo katika dakika ya sita ya
mchezo huo wakati Arnautovic alipoachia shuti la kiufundi la
kuzungusha lililompita kipa wa Chelsea Manuel Lanzini.
Baada ya kufungwa goli hilo timu ya
Chelsea ilijaribu kupambana vilivyo ili kurudisha goli hilo, lakini
jitihada zao ziligonga mwamba kutokana ngome ngumu ya mabeki wa West
Ham kuwa imara na pia kazi nzuri ya kipa Joe Hart.
Marko Arnautovic akiachia shuti na mpira kujaa wavuni na kuandika goli pekee katika mchezo huo.
Kocha mpya wa West Ham David Moyes akishangilia goli lililompa ushindi wa kwanza akiinoa timu hiyo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni