Kocha wa Tottenham Mauricio
Pochettino amewataka wachezaji wake kuendeleza wimbi la ushindi,
baada ya kuibuka na ushindi mnono wa magoli 5-1 dhidi ya Stoke City.
Katika mchezo huo Harry Kane
aliifungia Spurs magoli mawili na kuifanya kwenda mapumziko ikiwa na
magoli manne.
Son Heung-min alichangia goli la
kwanza ambalo Stoke walijifunga na kisha kuongeza goli la pili na
Christian Eriksen alifunga goli la tano kabla ya Shawcross kuwafuta
machozi Stoke.
Mshambuliaji Mkorea Son Heung-min akifunga goli la pili la Tottenhm
Harry Kane akiwa ameruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli la tatu la Tottenham
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni