Mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mara
tano Cristiano Ronaldo amefunga magoli mawili wakati Real Madrid
ikiipa kipigo kizito cha magoli 5-0 Sevilla.
Katika mchezo huo Real Madrid
ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa Nacho kwa shuti la karibu,
kisha Ronaldo akaongeza goli la pili.
Ronaldo tena akafunga kwa mkwaju wa
penati na Toni Kross akafunga goli nne na kutengeneza goli la tano
lililofungwa na Achraf Hakimi.
Mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora Duniani Cristiano Ronaldo akifunga goli katika mchezo huo
Kabla ya mchezo huo Cristiano Ronaldo alionyesha tuzo zake zote tano alizonyakua
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni