Kocha Antonio Conte ametetea kauli
yake ya kuwa Chelsea imetoka katika mbio za ubingwa, hata baada ya
kikosi chake kuifunga Huddersfield magoli 3-1.
Chelsea ilikosolewa baada ya
kufungwa na West Ham jumamosi, na kumfanya kocha Conte kukiri kuwa
haipo tena kwenye mbio za ubingwa wa msimu huu.
Hata hivyo jana Chelsea imefikisha
pointi sawa na Manchester United iliyo nafasi ya pili baada ya kupata
ushindi wa magoli yaliyofungwa na Tiemoue Bakayoko, Willian na Pedro.
Tiemoue Bakayoko akiangalia mpira alioupiga ukigongwa na kujaa wavuni
Mshambuliaji Mbrazil Willian akiwa ametikisa nyavu na kuifungia Chelsea goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni