Kocha Roy Hodgson amesema matatizo
ya kikosi chake cha Crystal Palace bado hayajaisha licha ya kupata
ushindi wa dakika za mwisho wa magoli 2-1 dhidi ya Watford.
Mchezo huo ulibadilika baada ya
mchezaji wa Watford, Tom Cleverley kutolewa nje kufuatia kupewa kadi
ya pili ya njano katika dakika ya 87.
Bakary Sako aliisawazishia Palace
dakika mbili baadaye kabla ya James McArthur kufunga goli la ushindi
kufuatia krosi iliyopigwa na Wilfried Zaha.
Kocha wa Burnley Sean Dyche amesema
soko ni kuwa na ndoto baada ya kikosi chake kukwea hadi katika nafasi
ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuifunga Stoke 1-0.
Mchezaji Ashley Barnes akiachai shuti na kufunga goli pekee katika dakika 71 akitokea benchi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni