.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 13 Desemba 2017

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI

Uongozi wa Mkikita ukiwa na uongozi wa kiwanda cha Unga cha Ukaya, Mkuranga, Pwani, ulipotembelea kiwanda hicho ambacho wako mbioni kuingia mkataba wa kusaga mihogo ya wanachama wao kupata unga wa kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui, Mkurugenzi wa Kiwanda, Ibrahim, Meneja wa Kiwanda, Matanga na Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange.

                                                                   Na Richard Mwaikenda, Mkuranga.
UNGA wa muhogo unatumika kutengenezea kishungi cha kuwashia moto katika vibiriti.

Jambo hilo lilithibitishwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kusaga muhogo cha Ukaya, Mkuranga, Ibrahim mbele ya uongozi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) uliotembelea kiwanda hicho.

Alisema kuwa miongoni mwa wateja wakubwa wa unga wao ni Kiwanda cha kutengenezea vibiriti cha Kasuku kinachoutumia kwa kutengenezea kishungi cheusi cha njiti ya kibiriti kinachotumika kuwasha moto.

Uongozi wa Mkikita ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kissui S. Kissui na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Adam Ngamange ulitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuingia nao mkataba wa makubaliano ya kukitumia kusaga mihogo ya wanachama wao kupata unga utakaouzwa na katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ibrahim alisema unga pia hutumika kutengenezea dawa ya kuzuia kuhara, pombe, mafuta, chakula cha wanyama na binadamu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni