Kocha Arsene Wenger amesema Arsenal
haipaswi kupata majeruhi zaidi katika kipindi hiki cha michezo mingi
baada ya Olivier Giroud kuumia misuli wakishinda goli 1-0 dhidi ya
West Ham.
Wenger, ambaye alifanya mabadiliko
ya wachezaji 11 katika kikosi chake akijipanga kuwavaa Newcastle
jumamosi, alipata wakati mgumu kuipenya ngome ya wageni wao.
Lakini mshambuliaji wa Uingereza
Danny Welbeck alifanikiwa kuipenya ngome ya West Hama kabla ya
mapumziko akitumbukiza kimiani mpira wa krosi ya Mathieu Debuchy.
Danny Welbeck akifuga goli pekee katika mchezo huo wa kombe la Carabao
Kipa wa West Ham Joe Hart akiwa chini huku mpira ukiwa umetinga kwenye wavu wake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni