Kocha wa Manchester City Pep
Guardiola amesema anafuraha mno baada ya kikosi chake kutinga kwa
ushindi wa matuta 4-3 nusu fainali ya kombe la Carabao Cup dhidi ya
Leicester City.
Kipa Claudio Bravo aliyeokoa mikwaju
miwili ya penati dhidi ya Wolves katika raundi iliyopita jana pia
alipangua penati ya Riyad Mahrez na Jamie Vardy penati yake kugonga
mwamba.
Wenyeji ilibidi waende hadi dakika
za lala salama ili kukomboa goli moja walilofungwa na Bernardo Silva,
na alikuwa Jamie Vardy aliyesawazisha goli kwa mkwaju wa penati.
Mshambuliaji Jamie Vardy akifunga mkwaju wa penati uliofanya mchezo huo uende katika muda wa nyongeza na kuishia kwa matuta
Kipa wa Manchester City Claudio Bravo akipangua penati ya Riyad Mahrez
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni