Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp
ameitaka timu yake kuendeleza makali ya kufumania nyavu baada ya
kuichakaza Bournemouth magoli 4-0 na kukwea hadi nafasi ya nne ya
msimamo wa ligi.
Magoli ya Liverpool yalifungwa na
Philippe Coutinho, Dejan Lovren, Mohamed Salah na Roberto Firmino na
kuwaruka Burnley na Arsenal katika msimamo wa ligi ingawa ipo nyuma
pointi 18 nyuma ya vinara wa ligi Manchester City.
Philippe Coutinho akishangilia kwa kukimbia baada ya kufunga goli la kwanza
Dejan Lovren akiwa ameruka kichwa cha kuchupa na kufunga goli la pili la Liverpool
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni