Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho ameapa kuwa kikosi chake kitapambana hadi mechi ya mwisho,
baada ya kuifunga West Brom Magoli 2-1 na kuwa pointi 11 nyuma ya
vinara wa ligi Manchester City.
Katika mchezo huo Romelu Lukaku
alikuwa wa kwanza kufumania nyavu kwa mpira wa kichwa akiunganisha
krosi ya Marcus Rashford, likiwa ni goli lake la pili katika michezo
miwili mfululizo baada ya kuondoa gundu la kutofunga kwa muda.
Kinda Jesse Lingard aliongeza goli
la pili kabla ya mapumziko kwa shuti lililomgonga Ahmed Hegazi na
kumpoteza mahesabu kipa wa West Brom. Gareth Barry aliifungia West
Brom goli pekee la kufutia machozi.
Mshambuliaji Romelu Lukaku akiruka juu na kufunga goli kwa mpira wa kichwa
Jesse Lingard akifunga goli kwa shuti lililomgonga beki wa West Brom Ahmed Hegazi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni