Luis Suarez amefunga goli lake la
nane na la tisa la ligi katika msimu huu wakati Barcelona ikishinda
magoli 4-0 dhidi ya Deportivo, na angepata hat-trick iwapo ingetumika
teknolojia ya kuaini mpira uliokatiza mstari wa goli.
Suarez alifunga goli la kwanza
katika kipindi cha kwanza kabla ya Mbrazil Paulinho kuongeza goli la
pili katika dakika ya 41. Baada ya mapunziko Suarez aliongea goli
lake la pili na kisha baadaye Paulinho tena akafunga goli la nne.
Mshambuliaji nyota wa Barcelona Luis Suarez akifunga goli huku Lionel Messi akiangali
Luis Suarez akiupiga kimanjonjo mpira ambao ulivuka mstari wa goli lakini goli hilo likakataliwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni