Kocha Sam Allardyce ameanza kuinoa
Everton kwa ushindi wakati Gylfi Sigurdsson na Dominic Calvert-Lewin
wakifunga magoli katika kupindi cha pili na kuizamisha Huddersfield.
Allardyce, aliyeteuliwa kuinoa timu
hiyo kwa mkataba wa miezi 18 siku ya Alhamis, ameshuhudia kikosi
chake kikionyesha uimara hii leo licha ya kutokuwa na kiwango bora
cha kutandaza soka.
Kocha Sam Allardyce akinyoosha mkono juu kuashiria mambo safi baada ya ushindi
Katika mchezo mwingine Demarai Gray
alifunga goli pekee la ushindi la Leicester City kufuatia krosi Riyad
Mahrez na kukosa nafasi ya kufunga goli la pili katika kipindi cha
pili wakizamisha Burnley.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni