Timu ya Manchester United imevunja
mwiko wa Arsenal kutofungwa nyumbani kwao katika msimu huu tangu
Januari mwaka huu baada ya kuitundika magoli 3-1 katika dimba la
Emirates.
Katika mchezo huo Antonio Valencia
alikuwa wa kwanza kufunga goli baada ya kunasa pasi isiyonamacho ya
Laurent Koscielny na kupachika goli kwa mpira uliompita tobo kipa wa
Arsenal.
Jesse Lingard alifunga goli la pili
baada ya kugongeana vyema na Romelu Lukaku na Anthony Martial,
Alexandre Lacazette akaifungia Arsenal goli kisha Lingard akatupia la
tatu.
Antonio Valencia akifunga goli kwa shuti kali lililompita tobo kipa wa Arsenal Petr Cech
Alexandre Lacazette akifunga goli pekee la Arsenal katika mchezo huo baada ya mabeki wa Manchester United kudhani ameotea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni