Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho amesema matumaini ya kikosi chake katika mbio za ushindi ni
kama yametoweka baada ya refa Michael Oliver kuwanyima penati wakati
wakipoteza kwa magoli 2-1 dhidi ya Manchester City.
Kwa matokeo hayo kikosi hicho cha
Pep Guardiola kinaongoza Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi
11 na Manchester City kuwa timu ya kwanza kushinda michezo 14
mfululizo katika msimu mmoja.
Katika mchezo huo wageni Manchester
City walikuwa wakwanza kufunga goli kupitia mchezaji bora wa mchezo
huo David silva, lakini makosa ya beki Nicolas Otamendi yalimfanya
Marcus Rashford asawazishe, hata hivyo Otamendi akaongeza goli la
pili na kufuta makosa yake.
Mchezaji David Silva akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Marcus Rashford akiachia shuti na kufunga goli pekee la Manchester United
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni