Mfaransa Paul Pogba ataanza katika
mchezo wa Manchester United dhidi ya CSKA Moscow hii leo, lakini
ataikosa Manchester City jumamosi baada ya kocha Jose Mourinho kuamua
kutoikatia rufaa kadi yake nyekundu.
Pogba alijikuta akilambwa kadi
nyekundu baada ya kumchezea rafu Hector Bellerin wa Arsenal siku ya
jumamosi wakati Manchester United ikiibuka na ushindi wa magoli 3-1,
na sasa atakosa mechi tatu za Ligi Kuu ya Uingereza.
Paul Pogba akifurahi jambo wakati akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Manchester United kujianda kuwavaa CSKA Moscow
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni