Sanamu ya Lionel Messi iliyopo
katika Jiji la Buenos Aires nchini Argentina imeharibiwa kwa mara ya
pili.
Sanamu hiyo ya nyota huyo wa
Barcelona ilizinduliwa Juni mwaka 2016 huko Paseo de la Gloria na
kuhudhuriwa na nyota kadhaa wa Argentina.
Mapema Januari sanamu hilo
lilikumbwa na waharibifu kwa mara ya kwanza na kukatwa kiunoni, na
safari hii limekatwa usawa wa enka.
Sanamu ya nyota wa Argentina Lionel Messi inavyoonekana baada ya kuharibiwa na watu wasiojulikana
Kushoto sanamu ya Lionel Messi ilivyokuwa imeharibiwa mara ya kwanza na kulia ilivyoharibiwa mara ya pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni