Alhamisi, 14 Desemba 2017
MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI DKT KIGWANGALLA AKABIDHI PIKI PIKI 19 MBELE YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA KWA WATENDAJI NA VIONGOZI WA KATA WA JIMBO HILO
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla leo amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi na Watendaji wa kata 19 ndani ya jimbo hilo,makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Check Pointi mara baada ya mkutano Mkuu wa jimbo kufanyika.Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana (Wa tatu kushoto) na kulia ni Katibu wa CCM wilaya Nzega Ndugu Janath Kayanda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngapula . Picha na Michuzi Jr-Nzega.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza mmoja wa Watendaji Kata kwa kukabidhiwa Piki Piki na Mbunge wao wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,jioni ya leo katika ukumbi wa Checki Point,mjini humo mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa cha cha Mapinduzi (CCM ) Ndugu Abdulrahaman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo la Nzega vijijini mapema jioni ya leo katika ukumbi wa mikutano wa Check Point,wilayani humo mkoani Tabora.Ndugu kinana amewapongeza Wana CCM wa jimbo la Nzega kwa kushinda uchaguzi wa marudio wa madiwani,viongozi mbalimbali walioshinda nafasi mbalimbali za uongozi kwa ngazi ya Wilaya na kuwataka kuwa wamoja sambamaba na kushirikana katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi na sii kulumbana tena.Picha na Michuzi Jr-Nzega.
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza mbele ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo hilo waliojitokeza kwa wingi,katika Mkutano wao Mkuu wa jimbo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana .Dkt Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi na Watendaji wa kata 19 ndani ya jimbo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngapula kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora,akitoa salamu mbele ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini kabla ya Mkutano Mkuu wa jimbo hilo kuanza.
Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwasalimia kabla ya kuanza rasmi mkutano mkuu wa jimbo hilo,ambapo Mbunge wa jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi wa Kata na Watendaji ili kuwasaidia kupambana na chanagamoto za usafri wakati wakiendelea kusikiliza na kutatua matatizo ya Wananchi wa jimbo hilo.
Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia mapema leo katika ukumbi wa Checki Point,mjini humo wakati wa mkutano mkuu wa jimbo hilo,ambapo Mbunge wa jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi wa Kata na Watendaji ili kuwasaidia kupambana na chanagamoto za usafri wakati wakiendelea kusikiliza na kutatua matatizo ya Wananchi wa jimbo hilo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni