Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho amesema kuwa angekuwa kwenye mapumziko nchini Brazil ama Los
Angeles iwapo angekuwa anafikiri mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya
Uingereza zimeisha.
Mourinho ametoa kauli hiyo baada ya
kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Bournemouth, goli
lililofungwa na mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku kwa mpira wa
kichwa kufuatia krosi ya Juan Mata.
Romelu Lukakku akiangalia mpira alioupiga kwa kichwa ukielekea kutinga wavuni kwenye kona ya juu ya goli
Tottenham imekwea katika nafasi ya
nne ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupata magoli mawili kupitia
kwa Serge Aurier na Son Heung-min na kuipa ushindi dhidi ya timu
ngumu ya Brighton katika dimba la Wembley.
Katika michezo mingine ya Ligi Kuu
ya Uingereza Arsenal imejikuta ikitoa sare tasa ugenini dhidi ya West
Ham nayo Liverpol ikashindwa kutamba nyumbani baada ya kulasimishwa
sare tasa na West Brom.
Mchezaji wa Liverpool Dominic Solanke akishangilia goli hata hivyo lilikataliwa na refa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni