Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa muda wa CWT, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, pamoja na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiimba wimbo wa mshikamano pamoja na Wajumbe wote wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia na kufungua mkutano huo wa CWT katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wajumbe wa CWT katika ukumbi wa Chimwaga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza viongozi wa muda wa Chama cha Walimu Tanzania walipokuwa wakiwasilisha hoja zao mbalimbali zinazo wakabili walimu nchini katika mkutano mkuu wa CWT uliofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. PICHA NA IKULU
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni