Katika hotuba ya Rais wa Palestina Mheshimiwa “Mahmuud Abbas”, ametahadharisha ya kwamba hakuna amani wala utulivu utakayopatikana katika eneo la mashariki ya kati bila ya kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa dola ya Palestina.
Aidha, Rais Abbas amelielezea azimio la Trump kuwa ni uhalifu mkubwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kimataifa na mikataba iliyosainiwa, huku akilizingatia azimio hilo kuwa ni sawa na lile “Azimio la pili la Balfour”.
Rais Abbas ameweka wazi kwamba, Marekani imeshusha ustahiki wake katika mchakato wa kisiasa kwa sababu ya kupendelea kwake kote kwa Israeli, huku akiashiria kwamba azimio la Trump halitoipa Israeli uhalali wowote mjini Jerusalem. Rais Abbas ametoa wito kwa Mkutano huo, kufafanua uhusiano wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu “OIC” na nchi nyingine duniani, kuhusiana na nafasi yake juu ya maazimio ya Trump.
Rais Abbas pia ametaka kuchukuliwa maazimio yanayoilazimisha Israeli kutekeleza maazimio ya kimataifa kuhusu Palestina, huku akiitaka dunia Kuangalia upya kuitambua kwake Israeli, muda wa kuwa inaendelea kukiuka sheria za kimataifa.
Rais wa Palestina ameshukuru misimamo ya awali ya Chuo Kikuu Kitukufu Cha Azhar na Papa Francis kuhusu Jerusalem,kama alivyowashukuru wananchi wake wakiwemo wakristo na waislamuwalio ndani na nje ya mji wa Jerusalem, ambao ndio wanaoutetea Msikiti wa Aqsana Kanisa la Ufufuo:
Rais wa Palestina ameshukuru misimamo ya awali ya Chuo Kikuu Kitukufu Cha Azhar na Papa Francis kuhusu Jerusalem,kama alivyowashukuru wananchi wake wakiwemo wakristo na waislamuwalio ndani na nje ya mji wa Jerusalem, ambao ndio wanaoutetea Msikiti wa Aqsana Kanisa la Ufufuo:
“Ninawaambia kwamba, hakika sisi tutaendelea kuwa pamoja na tukiwa sawa katika kuitetea Jerusalem, huku tukiwa tumethibiti kukabili njama ambazo zinalenga mji wetu na mji mkuu wetu,hadi tupate uhuru wetu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni