.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 15 Desemba 2017

SERIKALI YA KUWEIT YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akipokea zawadi na Vifaa kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar kutoka kwa Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jasem Al – Najem.
Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jasem Al – Najem akisisitiza umuhimu wa Nchi yake kuendelea kusaidia huduma za Kijamii Nchini Tanzania hasa kwa Watu wenye mahitaji Maalum.
Balozi Seif Kulia akiushukuru Ubalozi wa Kuweit Nchini Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kusaidia huduma za Kijamii Nchini Tanzania.
Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jasem Al – Najem Kushoto akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika hafla maalum ya makabidhiwano ya zawadi ya Vifaa kwa ajili ya Watu wenye ulemavu.
Baadhi ya Watu wenye mahitaji maalum pamoja na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakifuatilia matukio yaliyjiri kwenye hafla maalum ya makabidhiwano ya zawadi ya Vifaa kwa ajili ya Watu wenye ulemavu.
Balozi Seif kati kati akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jasem Al – Najem mara baada ya makabidhiano ya zwadi ya Vifaa kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu.
Baadhi ya Zawadi ya Vifaa vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuweit Nchini Tanzania kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

Serikali ya Kuweit imeihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kuiunga mkono katika harakati zake za kuimarisha ustawi wa Wananchi wake pamoja na miradi ya maendeleo.

Hatua hiyo itakwenda sambamba na Mpango Maalum uliobuniwa na Ofisi ya Ubalozi wa Kuweit Nchini Tanzania katika kusaidia Vifaa pamoja na zana za Kisasa zitakazowawezesha Watu wenye ulemavu kutengeneza vitu vya sanaa katika kiwango cha Kitaalamu.

Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jassem Al – Najem alitoa kauli hiyo wakati akikabidhi zawadi ya Vifaa vya Viti, Magongo, Miwani Pamoja na Mbao za kusomea kwa ajili ya Wananchi wenye mahitaji maalum Zanzibar hapo Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

Zawadi hizo alizokabidhiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi imegharimu Dola za Kimarekani Laki Tano sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 1.1.

Balozi Jassem alisema jitihada zinazochukuliwa na Kuweit katika kusaidia huduma za Kijamii katika Mataifa Rafiki yale yenye mahitaji maalum alizieleza kuwa zitakuwa endelevu.

Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania kupitia shughuli hiyo maalum alitoa mkono wa pole kwa Wanzania na Watanzani wote kufuatia vifo vya Askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { jwtz} waliouawa huko DRC.

Balozi Jassem alisema kitendo kilichofanywa na waasi wa ADF hakikubaliki kabisa Kimataifa kwa vile kimekwenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa na Umoja wa Amani katika maeneo yanayopatiwa ulinzi wa amani.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufuatia zawadi hiyo ya Serikali ya Kuweit Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Vifaa hivyo ni mkombozi mkubwa kwa Watu wenye Ulemavu hapa Zanzibar.

Balozi Seif alisema Watu wenye ulemavu hawakujitakia kuwa na maumbile waliyokuwa nayo bali ni kudra tuu za Mwenyezi Muungu ambazo wanapaswa kuendana nazo katika misingi na utaratibu wa ustahamilivu.

Alisema Jamii inapaswa kutambua kuwa na wao ni walemavu watarajiwa. Hivyo alisisitiza umuhimu wa Wananchi kuendelea kuwaenzi na kuwatunza Watu wenye Ulemavu bila ya ya kuwabagua kwani kufanya hivyo ni kujiingiza katika dhambi zinazopaswa kulaaniwa.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
15/12/2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni