.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 15 Desemba 2017

TANESCO MKOA WA SINGIDA YATARAJIA KUTUMIA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 549.5 KUKAMILISHA MIRADI 23

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Singida,Mhandisi Gamba Mahuggila akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari ofisini kwake kuhusu mafanikio ya shughuli zilizotekelezwa na zinazotarajiwa kutekelezwa na shirika hilo Mkoani Singida.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

SHIRIKA la Ugavi umeme nchini (TANESCO) Mkoa wa Singida linatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni 549.5 kwa ajili ya kugharamia ukamilishaji wa miradi 23 ya umeme kwa kuboresha miundombinu ili kukidhi mahitaji wateja,kufanya ukarabati, kuongeza nguvu ya umeme pamoja na miradi mipya.

Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ofisi za shirika hilo,Meneja wa TANESCO Mkoa wa Singida,Mhandisi Gamba mauggila alisema utekelezaji wa miradi hiyo yote mpaka sasa umefikia asilimia sabini.

Aidha Mhandisi Mauggila alibainisha kwamba kuna mradi wanaotegemea kuutekeleza na tayari wameshaufanyia uchambuzi wa kuhakikisha kwamba mji wote wa Singida unapatiwa umeme wa uhakika.

“Mpango huo upo katika hatua za awali naamini mpango utakapokuwa umekamilika tutawaita na kuwataarifu mipango hii inakwenda vizuri,na tunahakikisha kwamba mji wa Singida utapewa umeme kwenye maeneo yake yote.”alisisitiza Meneja huyo wa TANESCO.

Kwa mujibu wa Meneja huyo kuna sehemu 15 ambazo maeneo yake yanahitaji huduma za umeme na kuyataja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pamoja na Kimpungua,NHC,VETA na mengine yanayokuwa kwa haraka yatapatiwa pia umeme wa uhakika katika siku za karibuni.

Kuhusu suala la Mkoa wa Singida kuongeza huduma kwa wateja Meneja huyo aliweka bayana pia kwamba wameshafungua ofisi ndodgo ndogo kutekeleza agizo la serikali,kwenye maeneo ya Mji mdogo wa Shelui,Ndago na Mitundu.

Injinia huyo hata hivyo alisema pamoja na kufungua ofisi kamili kwa kuziongezea uwezo kama vile Mkalama ambayo wameshapata Meneja na hivi sasa wanafanya utaratibu wa kuongeza wafanyakazi ili ofisi hiyo ya wilaya iweze kujitegemea kwa kila kitu na Ofisi ya Itigi baada aya kupata kiongozzi wake muda wowote ule wataigeuza kuwa ofisi ya wilaya.

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO0 Mkoa wa Singida limeongeza wateja kutoka wateja 26,000 mwaka 2015 mpaka kufikia wateja 34,000 na wanataraajia kuwa na wateja 36,000 ifikapo julai,mwaka 2018.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni