Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Kassim, ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, ambapo ofisi hizo sasa ni rasmi kuendesha shughuli za Umoja wa Mataifa kutokea mkoani Dodoma. Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith S. Mahenge, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez; Mwakilishi wa Nchi wa UNICEF, Bi.Maniza Zaman, wafanyakazi wa UN, maofisa wa Serikali na wanafunzi walioalikwa kutoka shule mbalimbali za mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati wa tukio hilo; Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Rodgriguez, alisema, “Uzinduzi wa ofisi hii utawezesha na kukuza ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na Serikali hasa katika kipindi hiki muhimu Serikali inapohamia Dodoma.
Umoja wa Mataifa hufanyakazi kwa karibu na Serikali, na ofisi hii ni hatua ya kwanza katika Umoja wa Mataifa kuhamia Dodoma.”
Akitoa shukrani zake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Maniza Zaman, alisema mashirika ya Umoja wa Mataifa hushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuunga mkono mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano kupitia Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni