Kocha wa Chelsea Antonio Conte
amesema kiwango cha timu yake kimesahaulika kutokana na rekoni
inazovunja Manchester City, kauli aliyoitoa baada ya Chelsea kuifunga
Southampton goli 1-0, na kushinda michezo nane kati ya kumi ya Ligi
Kuu ya Uingereza.
Goli pekee la ushindi katika mchezo
huo lilifungwa na Marcos Alonso kwa shuti zuri na kuifanya Chelsea
kufikisha pointi sawa na Manchester United iliyokatika nafasi ya pili
ambayo inashuka dimbani leo dhidi ya West Brom.
Kipa wa Southampton akiruka bila mafanikio kuufuata mpira uliopigwa na Marcos Alonso
Kocha wa Newcastle Rafael Benitez
amesema anahitaji kufanya kitu Januari, baada ya kuporomoka katika
nafasi ya kushuka daraja baada ya jana kufungwa goli 1-0 na Arsenal.
Arsenal ilipata ushindi huo kupitia
goli zuri la Mesut Ozil katika kipindi cha kwanza na lilitosha kabisa
kwa kikosi cha Arsene Wenger kuibuka na ushindi.
Mjerumani Mesut Ozil akiachia shuti na kufunga goli pekee la Arsenal katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni