Cristiano Ronaldo amefunga goli la
ushindi kwa mkwaju wa mpira wa adhabu wakati Real Madrid ikiweka
rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutetea Kombe la Dunia kwa vilabu
baada ya kuifunga Gremio ya Brazil goli moja bila.
Ronaldo aliyeshinda tuzo ya Ballon
d’Or mwezi huu na kujitangaza kuwa ni mchezaji bora katika
historia, huku baadhi ya watu wakimbeza, lakini inaonekana anaendelea
kuziba midomo wanaompinga kwa kutwaa makombe.
Kwa goli hilo la Ronaldo, 32,
linamfanya kufikisha magoli 7 katika michuano hiyo sawa na mfalme wa
soko duniani Pele aliyefunga idadi kama hiyo ya magoli katika
michuano hiyo wakati huo ikijulikana kama kombe la mataifa.
Cristiano Ronaldo akipiga mpira wa adhabu ulioipatia ushindi Real Madrid na kutwa kombe la dunia
Kipa wa Gremio akiruka bila ya mafanikio kuufuata mpira wa adhabu uliopigwa na Ronaldo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni