Kocha Pep Guardiola amesema Kevin de
Bruyne anaisaidia Manchester City kuwa taasisi bora, baada ya
kuonyesha kiwango cha kuvutia katika ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya
Tottenham na kuongoza Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi 14.
Ilkay Gundogan akiziba nafasi ya
David Silva alioukosa mchezo huo, aliifanya Manchester City kuongoza
katika dakika ya 14, kabla ya baadaye mchezaji bora wa mchezo huo
Kevin De Bruyne kufunga kwa mpira wa shuti kali.
Gabriel Jesus aligonga mwamba kwa
shuti la mkwaju wa penati lakini Raheem Sterling aliuwahi mpira na
kutumbukiza mpira wavuni, Sterling tena akatumia makosa ya Eric Dier
na kufunga goli la nne na Christian Eriksen kuchomoa moja dakika za
mwisho.
Ilkay Gundogan akifunga kwa mpira wa kichwa wa kuchupa akiunganisha kona la Leroy Sane
Raheem Sterling akifunga goli lake kati ya mawili aliyoyafunga katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni