Wayne Rooney amesema Everton
imerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kutokea nyuma dhidi ya
Swansea City na kushinda magoli 3-1 ikiwa chini ya kocha wao mpya Sam
Allardyce.
Dominic Calvert-Lewin alitumbukiza
kimiani mpira uliorudi kufuatia penati ya Rooney iliyogonga mwamba na
kusawazisha goli la Leroy Fer aliyeifungia Swansea goli la kwanza.
Shuti la masafa la Gylfi Sigurdsson
dhidi ya timu yake ya zamani lilifanya Everton iongoze kabla ya
Rooney kufunga kwa mkwaju wake wa pili wa penati.
Leroy Far akiifungia Swansea goli la kwanza katika dakika ya 35 ya mchezo
Dominic Calvert-Lewin akiwahi mpira wa penati ya Rooney uliogonga mwamba na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni