Mhe. Waziri Mhandisi Kamwele, (wapili kushoto), Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo wakimsikiliza Mkandarasi, Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India.
Mhe. Waziri Kamwele, (kushoto), akifafanua jambo, wakati akipatiwa maelezo na Mkandarasi kutoka kampunin ya India ya WAPCOS, Mhandisi P.G. Rajani
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, ameanza ziara ya siku mbili ya kukagua baadhi ya miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2017.
Katika siku yake ya kwanza ya ziara hiyo, Waziri alitembelea Mradi wa Uboreshaji Mfumo wa Usambazaji maji ambapo kazi zinazofanyika chini ya mradi huo ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3.0 hadi milioni 6.0, lakini pia ujenzi wa vituo vine(4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa 16 za kusukuma maji, ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji yatakayokuwa na urefu wa kilomita 477.
Mradi huu utanufaisha maeneo ya Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni , Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo,Kitopeni, Ukuni, Kerege, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa maji wa Ruvu Chini.
Aidha maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba,Mbezi, Makuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo yote haya hupata huduma kutoka Mtambo wa Ruvu Juu ambao ulizinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhurim ya Muungani wa Tanzania Juni 21, 2017.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni