Cristiano Ronaldo amefunga mikwaju
ya penati miwili katika kipindi cha kwanza na kuisaidia Real Madrid
kuifunga Valencia magoli 4-1 na kupunguza presha ya kutimuliwa kocha
wao Zinedine Zidane.
Ushindi huo unaifanya Real Madrid
kupunguza pengo lake na wenyeji Valencia kuwa tofauti ya pointi mbili
tu, ikiwa na mchezo mmoja mkonono, ingawa bado ipo nyuma kwa pointi
16 na vinara wa La Liga Barcelona.
Valencia ilipata goli lake pekee
kupitia kwa Santi Mina, huku magoli mengine ya Real Madrid yakifungwa
na Marcelo na Toni Kroos kufunga goli la nne kwa shuti kali la masafa
dakika moja kabla ya mpira kumalizika.
Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo akifunga goli kwa mkwaju wa penati
Mjerumani Toni Kroos akiachia shuti kali na kufunga goli katika dakika ya 89
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni