Jay Rodriguez amefunga magoli mawili
wakati West Brom ikiishinda Liverpool kwa magoli 3-2 katika mchezo wa
Kombe la FA raundi ya nne uliotawaliwa na maamuzi ya kutumia msaada
wa video.
Refa Craig Pawson alikataa goli la
Albion, akaipa Liverpool penati na kuchelewa kwa dakika tatu kufanya
maamuzi ya kuwapati goli West Ham goli la tatu hadi aliposaidiwa na
refa anayetumia picha za video.
Rodriguez alifunga goli la
kusawazisha baada ya Firmino kuifungia Liverpool goli la kuongoza, na
kisha tena Rodriguez akaongeza goli la pili na kufanya matokeo kuwa
2-1. Joel Matib alijifunga goli la tatu baadaye Mohamed Salah
akafunga goli la pili la Liverpool.
Kipa wa West Ham Ben Foster akimdhibiti Mohamed Salah kufunga goli
Refa Craig Pawson akiomba msaada wa refa wa video baada ya kushindwa kufanya maamuzi
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp akiwa amechanganyikiwa na kipigo kutoka kwa West Ham
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni