Wakazi wa Mji wa Cape Town nchini
Afrika Kusini wametakiwa kuhifadhi maji kama vile maisha yao
yanategemea maji, ili kuepusha kufungwa kwa huduma ya maji.
Ukame mkali umelazimisha Manispaa ya
Jiji hilo kudhibiti matumizi kufikia lita 50 sawa na galoni 11 kwa
mtu mmoja kwa siku.
Maafisa wa Jiji la Cape Town
wamewasihi watu kuacha kutumia maji ya kuflash chooni, ili kuhifadhi
maji.
Mkuu wa serikali ya Mkoa wa Cape
Town amesema kuwa iwapo mabomba yatakosa maji itakuwa ni janga juu ya
janga.
Wakazi wa Jiji la Cape Town wakiwa kwenye foleni ya maji baada ya maji kuadimika
Wakazi wa Jiji la Cape Town wakiwa na madumu wakihaha kutafuta maji yaliyoadimika
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni