Mchezo wa kwanza wa Philippe
Coutinho katika La Liga akiwa na Barcelona umemalizika kwa ushindi wa
magoli 2-1 baada ya Barcelona kutokea nyuma na kuifunga Alaves.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester
City John Guidetti aliandika goli la kwanza kwa mpira uliomshinda
kipa Marc-Andre ter Stegen na kuwafanya wageni Alaves waongoze.
Luis Suarez aliisawazishia Barcelona
goli hilo na kisha baadaye Lionel Messi kuihakikishia ushindi kwa
goli la mpira wa adhabu.
Mpira wa adhabu uliopigwa na Lionel Messi ukielekea kuwapita mabeki na kujaa wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni