Manchester City imetinga kilaini
katika raundi ya tano ya Kombe la FA kwa kuibuka na ushindi wa magoli
2-0 dhidi ya timu ya Cardiff City.
Kevin de Bruyne aliipatia Manchester
City goli la kwanza katika kipindi cha kwanza na Raheem Sterling
akaongeza la pili kipindi cha pili.
Mpira uliopigwa na Kevin de Bryune ukitinga wavuni na kuandi goli la kwanza
Kocha Antonio Conte amemuelezea
Michy Batshuayi kama mchezaji kijana mwenye fursa ya kung'ara baada
ya kufunga magoli mawili, Chelsea ikishinda magoli 3-0 dhidi ya
Newcastle.
Mshambuliaji huyo Mbelgiji amekuwa
hapati nafasi katika kikosi cha Conte, ambaye alisema mchezaji huyo
anaweza kuondoka kwa mkopo mwezi huu. Marcos Alonso alifunga la tatu.
Mchezaji kijana wa Chelsea Michy Batshuayi akifunga goli kwa kuupiga mpira kwa kuubetua
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni