Ragnar Klavan amefunga goli katika
dakika za majeruhi na kuipatia Liverpool ushindi wa magoli 2-1 dhidi
ya Burnley.
Wenyeji Burnley walionekana kuwa
wangeambulia pointi moja baada ya Johann Gudmundsson kusawazisha
zikiwa zimebakia dakika tatu kabla ya muda wa kawaida kuisha.
Katika mchezo huo Liverpool ilikuwa
ya kwanza kupata goli kupitia kwa Msenegali Sadio Mane katika kipindi
cha pili kwa shuti zuri.
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane akifunga goli la kwanza la Liverpool
Ragnar Klavan akifunga goli la ushindi la Liverpool katika dakika za majeruhi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni