Manchester United imerejea katika
nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya
kupata ushindi mwepesi wa magoli 2-0 dhidi ya Everton katika dimba la
Goodison Park.
Kocha wa United Jose Mourinho
alikuwa akihaha kumaliza mfululizo wa sare tatu na alifanikiwa
kumaliza matokeo hayo licha kukabiliwa na upinzani kutoka kwa kikosi
butu cha kocha Sam Allardyce.
Anthony Martial alishuka dimbani
baada ya kukosekana kwa Romelu Lukaku na Zlatan Ibrahimovic na
kufanikiwa kufunga kwa shuti zuri la mpira wa kuzungusha na Jesse
Lingard akafunga la pili.
Mfaransa Anthony Martial akiachia shuti na kufunga goli la kwanza la Manchester United
Mpira uliopigwa na Jesse
Lingard (hayupo pichani) ukijaa wavuni na kumshinda kipa wa Everton
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni