.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Aprili 2018

IKULU YAIFUNDISHA NETIBOLI RAS IRINGA

 Kipa wa timu ya Uchukuzi, Willy Barton jana akidaka mpira katika mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa wakiajiandaa na mechi za mashindano ya Kombe la Mei Mosi yanayofanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. (Picha na Bahati Mollel-TAA)
 Mchezaji Sharifa Hamis (kulia) akifanya mazoezi ya kucheza bao na Ambakisye Mwasunga (kushoto) wakifanya mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Mei Mosi kwa upande wa michezo ya jadi inayofanyika kwenye uwanja wa Somora mkoani Iringa. Katikati ni mchezaji wa mchezo wa draft Bw. Omar Said akiangalia. (Picha na Bahati Mollel-TAA)
 Beki Nestory Tweve (3) wa timu ya Tumbaku ya Morogoro akitafuta njia ya kuwapita Francis Singa na Abdul Kawamba (wenye jezi nyeusi) wa RAS Iringa, katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora. Tumbaku walishinda magoli 3-0. (Picha na Bahati Mollel-TAA)

 Mshambuliaji Ramadhani Shegodo wa timu ya Tumbaku ya Morogoro, akipiga mpira ulioandikia bao la kwanza dhidi ya RAS Iringa, katika mchezo wa Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora. Tumbaku wameshinda mabao 3-0.
 Mfungaji Fatuma Machenga (GS) wa Ikulu akifunga mbele ya mlinzi wa RAS Iringa (GK), Maria Mwita katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) Iringa. Ikulu wameshinda magoli 49-8.
Mlinzi wa pembeni Ester Turuka (WA) wa RAS Iringa akirusha mpira kwa mfungaji wao Warda Sapal (GS) huku mlinzi Lilian Sylidion (GD) wa Ikulu akijitahidi kuzuia katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) Iringa. Ikulu wameshinda magoli 49-8.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni