Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara(VPL) msimu wa 2017/2018 kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo namba 178 utakaofanyika saa 10 jioni Kiingilio cha chini kitakuwa shilingi Elfu Saba(7,000) wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi Elfu Thelathini.
Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi Elfu Thelathini (30,000),VIP B na C shilingi Elfu Ishirini (20,000) na Upande wa Mzunguko kwenye viti vya rangi ya Chungwa,Bluu na Kijani itakuwa shilingi Elfu Saba (7,000)
Tiketi tayari zimeanza kupatikana kuanzia sasa kupitia Selcom
FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM(ASFC) KUPIGWA JUNI 2,2018 SHEIKH AMRI ABEID
Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) inatarajia kuchezwa Juni 2,2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha.
Katika mashindano ya ASFC mwaka huu kumefanyika maboresho ya kuongeza zawadi ambapo awali mshindi wa pili alikuwa hapati zawadi na katika msimu huu wa mashindano hayo mshindi wa pili atajikusanyia kiasi cha shilingi Milioni Kumi huku bingwa akibeba kitita cha shilingi Milioni Hamsini.
Zawadi nyingine zitakazotolewa ni pamoja na Mchezaji bora wa mashindano atakayezawadiwa shilingi milioni Moja,Kipa Bora atapata shilingi Milioni Moja huku mfungaji Bora pia akipata shilingi Milioni Moja wakati mchezaji Bora wa mchezo wa fainali akijizolea shilingi Laki Tano.
TFF YAVITAKA VILABU KUFUATA UTARATIBU,YASISITIZA HAITASITA KUVIKATA FEDHA KWA KUKIUKA MIKATABA.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) linavitaka vilabu vyote kuwa makini na mikataba wanayoingia na Wachezaji pamoja na makocha wao.
TFF haitasita kuzikata fedha klabu zote zitakazokuwa na madeni yanayodaiwa iwe kwa kukiuka mikataba yao na wachezaji,makocha au kwa namna nyingine yoyote.
Kumekuwa na klabu zinalalamika kinyume na utaratibu tunazitahadharisha kufuata utaratibu unaofahamika kinyume cha hapo hatutasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayekiuka utaratibu.
TFF inaendelea kusisitiza kwa klabu kutoa malalimiko yao kwa njia za kikanuni ili kuepuka hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi yao kama Ibara ya 50 ya katiba ya TFF inavyozungumza pamoja na Kanuni za Maadili.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni